ongoing MTWARA

USAFIRISHAJI WA MAZAO

USAFIRISHAJI WA MAZAO
Maendeleo100%

Usafirishaji Salama na Ufanisi wa Mazao kutoka AMCOS hadi Sokoni

MAMCU LTD inatoa huduma ya usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka kwenye AMCOS wanachama hadi kwenye maghala ya MAMCU kwa ajili ya kupokelewa, kupimwa, kukaguliwa ubora, kuhifadhiwa na hatimaye kuuzwa katika masoko mbalimbali.

Huduma hii inahusisha usafirishaji wa mazao kama korosho, ufuta, mbaazi, njugu na choroko, kwa kuzingatia usalama wa mazao na ufanisi katika mnyororo mzima wa thamani.

Malengo

Huduma zetu husaidia:

  • Kukusanya na kusafirisha mazao kutoka AMCOS hadi maghala ya MAMCU.

  • Kupunguza upotevu na uharibifu wa mazao baada ya mavuno.

  • Kuhakikisha mazao yanafika kwa wakati na katika hali nzuri.

  • Kurahisisha uhifadhi, upimaji na udhibiti wa ubora.

  • Kuwezesha usafirishaji wa mazao kutoka maghalani kwenda kwa wanunuzi.

  • Kuimarisha upatikanaji wa masoko na kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.

Faida

Mkulima → AMCOS → Ghala la MAMCU → Soko

Kupitia mfumo bora wa usafirishaji na usimamizi wa mazao, MAMCU LTD inaendelea kuwaunganisha wakulima na masoko, kulinda ubora wa mazao na kuimarisha maendeleo ya ushirika.

Picha za mradi

Shiriki Facebook LinkedIn WhatsApp